David Macharia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Embu baada ya kunywa pombe haramu ya kienyeji na kumeleta madhara makubwa yeye na wanywaji wenzake.
Zaidi ya watu 56 wamefariki Dunia na wengine zaidi ya 70 wana hali mbaya hospitali, baada ya kunywa pombe haramu za kienyeji katika miji minne tofauti huko nchini Kenya.
Matukio hayo yalitokea katika miji ya Embu, Kiambu, Kitui na Makueni.
Katika jimbo la Embu vifo vimeongezeka hadi kufikia 25, baada ya watu 11 zaidi kufariki dunia jana, na hii ni baada ya watu hao kunywa pombe haramu katika mtaa wenye makazi duni wa Shauri Yako.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni