Ofisa Masoko wa Msanii Day, Peter Mwendapole waliokaa wa kwanza kulia akiongea na waandishi wa habari juu ya siku hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa BASATA, Vivian Shalua akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk. Fenella Mukangara keshokutwa anatarajiwa kuzindua Siku ya Msanii Tanzania katika sherehe zitakazofanyika katika hoteli ya Sea Cliff Dar es Salaam.
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Mradi
wa Siku ya Msanii Tanzania, Petter
Mwendapole, alisema Dk. Mukangara amepewa jukumu hilo kutokana wizara yake
kuhusika moja kwa moja sanaa.
“Waziri amekubali jukumu la kuwa mgeni rasmi kwa sababu
wizara yake ndio mama wa wasanii, na anaelewa matatizo ya wasanii na amekubali
kuwa kulibeba jukumu hilo na atakuwepo na timu
nzima ya wizara,” alisema.
Mkurugenzi wa Masoko wa Basata wa Vivian Shaluwa alisema
siku ya Msanii ilibuniwa mwaka 2004 lakini Tanzania iliamua kuichukua na
kuianzisha mwaka 2008 lakini baada ya mchakato wa muda mrefu, kampuni ya Haak
Neel imepewa jukumu la kusimamia kazi hiyo.
“Siku ya Msanii itahusisha sanaa mbalimbali kuanzia urembo,
muziki wa dansi, uchoraji, unenguaji, lakini pia siku ya Msanii ambayo tamati
yake itakuwa Oktoba 25 itakuwa na tuzo za aina mbalimbali kutambua mchango
wao,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Haak Neel Production, Godfrey
Katula alisema kampuni yake imejiandaa vyema kusimamia shughuli hiyo na
kuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha wanatumia vyema siku ya Msanii katika
kutambulisha kazi.
“Haak Neel imejipanga kushirikiana na wasanii katika
kutambua siku yao, tumeona kuna siku ya wanawake duniani, kuna Mei Mosi, kwa
ajili ya wafanyakazi, kuna siku ya ukimwi kwa hiyo hii ni heshima kwa wasanii
kutambuliwa kwa siku yao.”
Mbali na viongozi wa BASATA, Kamati ya Siku ya Msanii
inahusisha wasanii kutoka sekta mbalimbali za sanaa ambao ni pamoja na Philemon
Mwasanga, Asia Idarous, Kimera Billa, Abdul Salvador, Adrian Nyangamale,
Sulemani Ling’ate.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni