Wapiganaji wa Taliban wametoa picha zinazoonyesha jinsi walivyomkabidhi mwanajeshi wa Marekani waliyekuwa wanamshikilia mateka kwa miaka mitano, Sajenti Bowe Bergdahl kwa kikosi cha jeshi la Marekani.
Katika picha hizo, anaonekana Bowe akiwa katika Pickup msituni mashariki mwa Afghanistan akisubiri kuja kuchukuliwa na helkopta ya jeshi la Marekani huku wapiganaji wa Taliban wakiwa wametapakaa sehemu mbalimbali za eneo hilo wakiwa na silaha nzito za kivita.
Mmoja wa wapiganaji wa Taliban akiwa amesimama kilimani huku amebeba silaha wakati wakisubiri kumkabidhi Bowe Bergdahl kwa wanajeshi wa Marekani waliofika kumchukua baada ya kumuachia huru toka mafichoni walikokuwa wakimshikilia kwa miaka mitano.
Kuachiliwa kwa Bowe kulifikiwa baada ya Marekani nayo kuwaachilia huru wapiganaji watano wa Taliban waliokuwa wakishikiliwa katika gereza la Guantanamo Bay.
Bowe akiwa amesimama pembeni ya mpiganaji wa Taliban akiiangalia helkopta ya jeshi la Marekani ( haionekani pichani ) wakati ikiwa inatua eneo alipochukuliwa.
Helkopta ya jeshi la Marekani ikiwa na wapiganaji wenye uzoefu wa hali ya juu wa kivita waliofika msituni mashariki mwa Afghanistan kumchukua Bowe ( mwenye kanzu nyeupe ) baada ya kuachiliwa huru na wapiganaji wa Taliban
Helkopta ya jeshi la Marekani ikiondoka baada ya kumchukua Bowe toka mikononi mwa wapiganaji wa Taliban msituni.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni