Wabunge wa Meru nchini Kenya
wanatarajia kugusia suala la kupigwa marufuku Mirungi kwenda
Uingereza watakapokutana na Rais Uhuru Kenyatta kwenye mkutano wa
wabunge wa Jubilee Ikulu hii leo.
Mwakilishi wa Wanawake wa Meru
Florence Kajuju ambaye anaongoza kamati ya bunge ya taifa
iliyoteuliwa kuchunguza jambo hilo amesema wabunge watajadili na rais
suala hilo.
Kajuju amesema kuna maswali mengi
hayajajibiwa kuhusu hatua ya serikali ya Uingereza kuzuia mirungi
kuingia nchi hiyo ya Ulaya, hivyo wanapaswa kuelezwa iwapo ni adhabu
kwa Kenya. Uingereza hivi karibuni iliingiza mirungi katika kundi la
dawa za kulevya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni