
Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba akitoka kukagua jukwaa lenye hadhi ya kimataifa la Ebony FM kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika jana kwenye viunga vya Samora mkoani Iringa. (Picha zote na Zainul Mzige)

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Tosamaganga wakiwasili kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio inayowalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 iliyozinduliwa rasmi jana mkoani humo.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari wakiwemo Shule ya wasichana Iringa wakiendelea kumiminika kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.

Stella Shubi kutoka Clouds Media (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika kwenye viwanja Samora mjini Iringa.

MC wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio B 12 kutoka Clouds FM Redio ambao ndio waratibu wa uzinduzi wa kampeni hiyo akiwa na mtoto aliyeashangaza umati wa vijana waliofurika kwenye uzinduzi huo baada ya kujibu swali ambalo hawakutegemea angelijibu kutokana na umri wake.

Meza Kuu, Kutoka kulia ni Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu pamoja na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni