Shirika la ndege la Uingereza, British Airways limesitisha safari zake zote za ndege kuelekea mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown pamoja na mji mkuu wa Liberia, Monrovia hadi hapo tarehe 31 mwezi huu wa nane.
Taarifa ya shirika hilo iliyotolewa na msemaji wake imesema kuwa, kufutwa kwa safari hizo ni kutoka na nchi hizo hivi sasa kukumbwa na ugonjwa wa Ebola.
Msemaji huyo amesema kusitishwa kwa safari hizo ni kwa ajili ya kulinda usalama wa abiria wao, wahudumu wa ndege pamoja na wafanyakazi wote wa shirika hilo.
Tayari ugonjwa huo wa Ebola umeshaua watu wapatao 880 katika nchi za Afrika Magharibi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni