.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Agosti 2014

COASTAL UNION YAMFUNGIA BANDA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA KUTOKUCHEZA SOKA NDANI NA NJE YA NCHI

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umemfungia aliyekuwa beki wa kushoto Abdi Banda kucheza mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kukosa nidhamu na kusaini mikataba katika vilabu viwili tofauti.

Adhabu hiyo itahusisha kutokucheza mechi zozote ikiwemo zile za kirafiki kutokana na kukiuka makubaliano aliyoingia na klabu hiyo ya Coastal Union wakati aliposajiliwa.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa uongozi umeamua kumpa adhabu hiyo kwa kukosa nidhamu pale aliposaini mkataba mwengine na timu ya Simba SC ya Dar es Salaam wakati akijua tayari ana mkataba wa miaka mitatu na timu ya Coastal Union.

El Siagi amesema kuwa mchezaji huyo alikuwa amebakiza miaka miwili kucheza timu ya Coastal Union na hivi sasa yupo katika mikataba miwili kwa timu mbili tofauti ambazo zinashiriki ligi moja.


Amesema kuwa kutokana na hali hiyo mchezaji huyo atakuwa amevunja sheria na kanuni za mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kulitaka shirikisho la soka kutoa ushirikiano katika maamuzi hayo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni