.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 31 Agosti 2014

LIGI KUU NCHINI UINGEREZA, WEST HAM YAFUNGWA 3-1 NA SOUTHAMPTON, QPR YATAMBA MBELE YA SUNDERLAND NA SWANSEA MOTO MKALI

Timu ya soka ya West Ham ikicheza nyumbani hapo jana ilijikuta ikikubali kipigo cha mabao 3-1 toka kwa Southampton katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza. 

Magoli ya Southampton yaliwekwa kimiani na mchezaji Morgan Schneiderlin aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 45 na baadaye akafunga tena bao pili katika dakika ya 68 na mchezaji Pelle akaifungia Sothampton bao la tatu nala ushindi katika dakika ya 83. 

Bao la West Ham lilifungwa na Mark Noble katika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza, Qeens Park Rangers ( QPR ) jana waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuifunga Sunderland bao 1-0 katika mchezo ulikokuwa na ushindani wa hali ya juu. 

Bao la QPR lilifungwa na mchezaji Charlie Austin.
Wao Swansea ambao walianza ligi kwa kuitandika Manchester United mabao 2-1, hapo jana waliendeleza makali yao katika ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuitandika West Brom mabao 3-0. 

Ikicheza kwa nguvu na kasi kubwa, Swansea walianza kuijpatia mabao yao katika dakika ya pili ya mchezo mfungaji akiwa ni Nathan Dyer ambaye aliifungia tena timu yake bao la tatu katika dakika ya 72. 

Bao la pili la Swansea lilifungwa na Routledge katika dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni