.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 19 Agosti 2014

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI AKUTANA NA MASHEIKH WA MIKOA NCHINI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiwa na Mufti na Sheikh mkuu wa Tanzania Shabani Simba na viongozi wengine wa dini ya kiislamu wakati wakiingia katika ukumbi wa bwalo la maafisa wa Polisi kuhudhuria kikao cha muendelezo wa kampeni ya familia yetu haina mhalifu kilichoratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka. Picha na Hassan Mdeme- wa Jeshi la Polisi.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na masheikh wa mikoa na maimamu wa misikiti katika ukumbi wa bwalo la maafisa wa Polisi wakati wa kikao cha muendelezo wa kampeni ya familia yetu haina mhalifu kilichoratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka. Picha na Hassan Mdeme- wa Jeshi la Polisi

                                                                          Na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi

Viongozi wa dini wametakiwa kuendelea kufanya doria za kimwili na kiroho katika kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwajenga vijana katika maadili mema na kuacha kutenda dhambi ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu alipokutana na viongozi wa dini ya kiislam katika ukumbi wa Bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es salaam. Kikao hicho kiliratibiwa na taasisi ya kiislamu ya Mwinyi Baraka inayoongozwa na Sheikh Issa othuman.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Mufti wa Tanzania Shabani Simba, Katibu mkuu wa Bakwata, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Masheikh wa mikoa ya Tanzania bara pamoja Maimamu wa Miskiti.

IGP Mangu alisema kuwa haijawahi kutokea kokote duniani kwa Polisi kula njama na viongozi wa dini katika kupambana na wahalifu na watenda dhambi, hivyo aliwaomba viongozi hao wa dini waongeze mahubiri yenye kuwataka waumini kutenda mema pamoja na kuongeza nguvu ya kuimarisha kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za kuabudia.

Naye, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Shaban Simba alisema kuwa dini zote zinahimiza waumini wake kutenda mema na kujiepusha kushiriki katika vitendo viovu, hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea kuwakamata wale wote watakaobainika kutenda uhalifu kwani hivi sasa uhalifu upo hata kwenye taasisi za dini.

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa mkoa wa Arusha Shabani Juma, wakati akitoa salamu za mkoa huo, alisema kuwa mkoa wa Arusha kwa sasa hivi upo shwari na wa amani, hivyo ni wajibu wetu kulinda amani tuliyonayo kwani ndio msingi wa kila kitu.

Kikao hicho ni muendelezo wa mkakati wa Jeshi la Polisi katika kuwajengea uwezo viongozi wa dini, ambapo viongozi hao wa dini waliazimia kwa pamoja kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kampeni ya kutengeneza familia zisizo na wahalifu kupitia mahubili yao pamoja na kuendelea kuimarisha kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada kwa rahisi ya mawasiliano katika kuwadhibiti wahalifu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni