.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 12 Agosti 2014

MUIGIZAJI NYOTA WA MAREKANI ROBIN WILLIAMS AFARIKI DUNIA

Muigizaji nguli wa filamu nchini Marekani Robin Williams amekutwa amekufa nyumbani kwake katika tukio ambalo linaaminika kuwa ni la kujiua.

Polisi wa Kaunti ya Marin wamethibitisha kifo cha muigizaji huyo nyota mwenye umri wa miaka 63, baada ya maafisa wa msaada wa dharura kufika nyumbani kwake jana mchana.

Williams alikuwa ni maarufu katika uigizaji kwenye filamu kama Good Morning Vietnam na Dead Poets Society na alishinda tuzo za Oscar kwa uhusika wake kwenye filamu ya Good Will Hunting.

Katika salamu zake za rambirambi Rais Barack Obama amesema Williams aliwafanya watu wacheke na aliwafanya watu walie katika uigizaji wake wakati wa uhai wake.
                             Mtoto akiweka maua mbele ya nyumba ya Robin Williams


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni