Polisi katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta wanamshikilia mwanaume mmoja raia wa
Taiwan baada ya kukutwa akiwa amebeba dola feki 250,000 zenye thamani
sawa na shilingi milioni 21.2 za Kenya.
Mtu huyo ambaye anaumri wa miaka 30, amekamatwa jana usiku akishuka kwenye ndege ya Shirika la
Ndege la Ethiopia iliyotokea Abu Dhabi, ambapo fedha hizo alikuwa
amezizungushia kwenye mfuko wa karatasi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni