.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Agosti 2014

SHIRIKA LA NDEGE LA MALAYSIA KUWAPUNGUZA KAZINI ZAIDI YA WAFANYAKAZI 6,000

Shirika la ndege la Malaysia liko mbioni kuwapunguza kazini zaidi ya wafanyakazi wake wapatao 6,000 ili kuweza kukabiliana na hali ngumu inayolikabili shirika hilo la ndege baada ya kukumbwa na majanga mawili makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. 

Mapema tarehe 08 mwezi machi mwaka huu moja ya ndege ya shirika hilo MH370 Boeing 777 ikiwa na zaidi ya abiria 239 ikitokea Kuala Lumpur kuelekea Beijing, China ilianguka kusini mwa bahari ya Hindi na tangu wakati huo haijaonekana wala abiria wake.

July 17'2014 ndege yake nyingine MH17 Boeing 777 ikiwa na abiria 298 ikitokea Amsterdam, Uholanzi kuelekea Kuala Lumpur ilitunguliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi wakati ikikatiza katika anga la Ukraine na kuua abiria wote. 

Hivi sasa Malaysia Airline inakabiliwa na hali ngumu ya kifedha baada ya kupoteza mvuto wake kwa wasafiri, na sasa shirika hilo litasimamiwa na serikali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni