.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 23 Agosti 2014

WAKATI KANSELA WA UJERUMANI AKIWASILI UKRAINE, MALORI YALIYOKUWA NA MISAADA YAGEUZA KUREJEA URUSI

 Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amewasili katika mji  mkuu wa Ukraine, Kiev tayari kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo, Petro Poroshenko. 

Kiongozi huyo ameonyesha kuiunga mkono Ukraine kufuatia mzozo unaondelea nchini humo na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
 Wakati Kansela Merkel akiwa na mazungumzo na rais wa Ukraine, malori yaliyokuwa yamebeba misaada toka Urusi yamegeuza na misaada hiyo kurejea Urusi. 

Zaidi ya malori 200 yameondoka mashariki mwa mji wa Luhansk ambao unadhibitiwa na waasi wanaoipinga serikali ya Ukraine.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni