.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 24 Agosti 2014

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA FUPI JIJINI MWANZA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa mbele ya kaburi la Vedasto Kitwanga,mtoto wa Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Wanne kulia) wakati alipokwenda nyumbani kwa Naibu Waziri huyo eneo la Usagara Mwanza August 23, 2014 kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae . Wengine pichani ni mke wa Naibu Waziri huyo, Matrida (wanne kushoto) na kushoto kwa Waziri Mkuu ni binti yao, Agness Misoji Kitwanga . Kulia ni Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga na Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Erasto Ndikilo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kulia) baada ya kuwasili nyumbani kwa Naibu Waziri huyo, eneo la Usagara, nje kidogo ya jiji la Mwanza ambako alikwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae Vedastus Kitwanga kilichotokea hivi karibuni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipigiwa magoti na Matrida Kitwanga (kulia) mke wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kulia) baada ya kuwasili nyumbani kwa Naibu Waziri huyo, eneo la Usagara, nje kidogo ya jiji la Mwanza ambako alikwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae Vedastus Kitwanga kilichotokea hivi karibuni. Katikati ni binti wa familia hiyo,Agnes Misoji Kitwanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wadau wa ujenzi wa jengo lenye Mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa Mwanza unaoboreshwa wakati alipofanya ziara ya kukagua maboresho ya uwanja huo August 23, 3024 Katikati ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dr. Charles Tizeba.(Picha na Ofisi ya Waziri MKuu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni