.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Septemba 2014

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AOMBA SAPOTI YA KUANDALIWA MECHI YA KUTETEA MKANDA WAKE WA WPBF AFRIICA

Na mwandishi wetu. 

Bondia Ibrahimu Class King Mawe anayeshikilia mkanda wa WPBF Afrika katika uzito wa Light welterweight amejitokeza hadharani na kusema mchezo wa ngumi nchin Tanzania haulipi kutokana na malipo yake kuwa madogo sana. 

Bondia huyo ameibuka na kutoa madai hayo baada ya kumpiga bondia Mwansa Kabinga.

Mpambano huo uliofanyika june 8 mwaka huu huko Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia na kuibuka mshindi katika raundi ya tisa, bondia huyo ana ndoto ya kuwa bingwa wa dunia katika miaka ya hivi karibuni.

Amesema mabondia wa hapa nchini bado hawajajielewa kutokana na kuto kuwepo na wafadhili wa kutosha katika mchezo wa masumbwi ila ufadhili mwingi unapelekwa katika mambo ya soka huku wakiuacha mchezo wa masumbwi hauna mwelekeo na sapoti yoyote.


Bondia huyo alijitamba kwa kujinasibu kuwa kwa hapa nchini hakuna bondia ambaye anaweza kumbabaisha katika kipindi hiki kwani yeye kwa sasa yupo matawi ya juu.

Bondia huyo anayefanya mazoezi katika kambi ya Ilala, ananolewa na jopo la makocha likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'

Ameomba watu mbalimbali kujitokeza kumsaidia ili atetee mkanda wake wa WPBF Africa alioupata Zambia ili awadhihirishie watu kuwa uwezo alionao ni mkubwa sana katika masumbwi, kingine ni wadhamini wajitokeze kumpa sapoti kwani ana uwezo wa kuwatangazia biashara mbalimbali ukizingatia yeye ni bingwa na bado kijana mdogo mwenye nia ya kufika mbali katika mchezo wa masumbwi nchini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni