.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Septemba 2014

CHIPPO ATAKA USHINDI MECHI YA SIMBA.

KOCHA MKUU wa Coastal Union ya Tanga, Yusuph Chippo amewapa mitihani mkubwa wachezaji wa kikosi hicho kuhakikisha wanapambana kufa na kupona ili kuweza kuchukua pointi tatu dhidi ya Simba Jumapili wiki hii.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya pazia la michuano ya Ligi kuu Tanzania bara kufunguliwa.

Chippo aMEsema maandalizi ya kuelekea mchezo huo kwa wachezaji wake yanaendelea vizuri kwa wachezaji wote kuhudhuria kwenye mazoezi ya timu hiyo ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya soka Disuza jijini Tanga na Popatlaly

Licha ya mazoezi hayo ya uwanjani wachezaji hao wamekuwa wakiingia gym asubuhi kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort huku walinda milango wa timu hiyo wakifanya mazoezi maalumu ya kuwawezesha kuwa imara zaidi.

Chippo amesema timu hiyo itaingia uwanjani hapo wakiwa na matumaini ya kupata ushindi wa aina yoyote ile ili kuweza kuanza ligi kuu vema lengo likiwa kuanza mikakati yao ya kuwania taji hilo ambalo linawaniwa na timu kumi na nne.
Hata hivyo Kocha huyo aliendelea kusisitiza nidhamu na kujituma kwa wachezaji hao ili waweze kupata mafanikio kwa sababu hiyo ndio silaha tosha ya kupata matokeo mazuri kwenye mechi yoyote ile.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO.
COASTAL UNION.
OFISA HABARI
OSCAR ASSENGA.
0714543839.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni