.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 24 Septemba 2014

KOCHA MKUU COASTAL UNION AWA MKALI

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Yusuph Chippo amewataka waandishi wa habari za michezo hapa nchini kuacha kupika stori kwenye vyombo vya habari badala yake waandika habari zilizokuwa na ukweli.

Hatua hiyo ya Kocha Chippo inatokana na taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti moja la michezo hapa nchini likimnukuu kocha huyo kusema kuwa tatizo la Simba lipo kwenye beki na watapata wakati mgumu watakapocheza na timu ambayo inawashambuliaji wenye kasi jambo ambalo hakulisema.

Chippo alisema kuwa kitendo hicho kimemshangaza sana kuona waandishi
wanaacha kufanya kazi zao kwa ueledi mkubwa kwa lengo la kuchochoea
kasi ya maendeleo ya soka nchini badala yake wamekuwa wamekuwa
wakitunga stori ambazo hazipo.

Alisema kubwa zaidi lililomshangaza ni kuona taarifa hiyo ikiandika
kuwa alisema kwa jinsi Simba inavyocheza itapata wakati mgumu
itakapocheza na Yanga, kiungo na washambuliajio wako vizuri lakini
beki yao ina tatizo hivyo wanahitaji kuangalia kwa umakini hasa
washambuliaji wa kasi.

Aidha alisema habari hizo hazifahamu wala hakuzungumza na mwandishi wa
aina yoyote ile hivyo kuwataka kuacha kufanya hivyo kwani
wanatengeneza masuala yasiyokuwa mazuri kwenye jamii hususani ya
wanamichezo hapa nchini.

“Tunafahamu kuwa waandishi wa habari wanakazi kubwa sana ya
kuielimisha jamii inayowazunguka hivyo nawasihi fanyeni kazi zetu kwa
ueledi mkubwa na kuacha kupika stori kwenye vyombo vyenu “Alisema
Chippo.

Hata hiyo alisema timu hiyo imeanza kuipiga mahesabu ya kuhakikisha
inachukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi
kuu soka Tanzania bara itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja
wa Sokoine Mbeya.

Chippo alisema kuwa kikosi chake kimekuwa na hari mpya hivyo
atahakikisha anawaanda vizuri wachezaji wake ili waweze kucheza
kandanda nzuri ambalo linawawezesha kupata mabao mengi kwenye mechi
hiyo.

Coastal Union tayari imekwisha kuwasili mkoani Mbeya ikijiandaa na
mechi yake dhidi ya Mbeya City itakayochezwa kwenye uwanja wa sokoine
mkoani humo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni