.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Septemba 2014

MKONGWE GABRIEL BATISTUTA ATAMANI AKATWE MIGUU YAKE KWA MAUMIVU


Mchezaji Nyota Mkongwe wa Argentina Gabriel Batistuta anadaiwa kumuomba daktari wake amkate miguu yake ili kumuepusha na maumivu makali aliyonayo tangu astaafu soka mnamo mwaka 2005.

Mshambuliaji huyo ambaye alicheka na nyavu mara 56 kati ya mechi 78 katika michuano ya kimataifa, anasumbuliwa mno na maumivu ya miguu kutokana na mikiki mikiki aliyokuwa akifanya dimbani katika kipindi cha miaka 17 ya soka.

Batistuta kwa sasa hawezi kutembea na hulazimika kujisaidia haja ndogo akiwa kitandani kutokana na kushindwa kabisa kunyanyuka na kutembea kwa kutumia miguu yake iliyo na maumivu makali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni