Wananchi wa Scotland watapiga kura
hii leo iwapo nchi hiyo ibakie kuwa chini ya Utawala wa Muungano wa
Kifalme ama iwe taifa linalojitegemea.
Wapiga kura watasema ndio ama hapana
katika kujibu swali la kura ya maoni, iwapo Scotland iwe taifa huru.
Watu 4,285,323 ambao ni asilimia 97
ya wapiga kura wamesajiliwa kupiga kura ambapo idadi kubwa
inatarajiwa kujitokeza kupiga kura na matokeo yake kutolewa kuanzia
kesho asubuhi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni