BONDIA Said Mbelwa mwenye rekodi yakushinda 27,kupigwa 16 na drawn 4 ambapo ana jumla ya mapambano 48 aliyocheza ameapa kumchakaza mpinzani wake george Dimoso mwenye rekodi yakushinda mapambano 11 kupigwa ,10 ,drawn 2 na jumla ya michezo aliocheza ni 23 siku ya October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam
Akizungumzia mpambano huo Mbelwa ambaye alikuwa kimya kidogo mda mrefu kutokana na kufungiwa baada ya kumpiga bondia Kalama Nyilawila kwa kupiga mateke wakati wa mpambano wao uliofanyika uliofanyika may 24
unajua kipindi chote nilichokuwa nje ya uringo nilikuwa nafanya mazoezi ya nguvu hivi sasa nipo fiti sana hivyo namtahazalisha Dimoso kuwa nayeye afanye mazoezi ya kutosha vinginevyo siku hiyo ataondoka uringoni ajitambui
Nae mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine kati ya Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
Pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hassani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
Siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni