.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

COASTAL UNION WAANZA MAANDALIZI YA MECHI YAO DHIDI YA NDANDA SC. TANGA.

TIMU ya Coastal Union ya Tanga jana imeendelea na mazoezi yake kwenye uwanja wa shule ya sekondari Popatlaly ikijiandaa na mechi yake dhidi ya Ndanda SC itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani wikiendi hii.

Mazoezi hayo yaliyoanza saa kumi jioni na kumalizika saa kumi na mbili jioni yakisimamiwa na Kocha Mkuu Yusuph Chippo akiwa na Msaidizi wake,Benard Mwalala sambamba na Mkurugenzi wa Ufundi Mohamed Kampira.

Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi hayo,Kocha Chippo amesema maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yanaendelea vema na hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi.

Chippo amesema kutokana na juhudi zinazofanywa na wachezaji kwenye mazoezi hayo wanamatumaini makubwa ya kuchukua pointi tatu muhimu kwenye mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza kucheza nyumbani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni