Bao pekee lililofungwa kwa kichwa na
Cristiano Ronaldo katika dakika ya 95 limeiwezesha Ureno kuibuka na
ushindi ugenini dhidi ya Denmark katika mchezo wa kuwania kufuzu
michuano ya Mataifa ya Ulaya.
Ronaldo aliruka juu na kuiunganisha
krosi iliyopigwa na Ricardo Quaresma na kuutumbukiza mpira wavuni
uliompita kipa Kasper Schmeichel na kufanya Ureno kutoka na pointi tatu
katika mchezo huo uliochezwa Copenhagen.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni