Daktari wa Jijini New York nchini
Marekani aliyerejea kutoka nchi ya Guinea iliyokumbwa na ugonjwa wa
Ebola amebainika kuwa na virusi vya Ebola.
Dktari huyo Craig Spencer, aliyekuwa
anawatibu wagonjwa wa Ebola wakati akifanya kazi na shirika la
misaada la Madaktari wasio na Mipaka (MSF), alifika New York akiwa na
homa siku ya Alhamisi.
Tukio hili la mgonjwa wa Ebola ni la
kwanza kutokea Jijini New York, na ni mgonjwa wa nne kutokea nchini
Marekani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni