Wanainchi wa Msumbiji leo wamepiga
kura katika uchaguzi ambao umetajwa kuwa mtihani mgumu kwa chama
tawala cha Frelimo, chama ambacho kimelitawala taifa hilo tajiri
lenye rasilimali nyingi tangu lilipopata uhuru mwaka 1975.
Wapiga kura walionekana wakiwa
katika misitari mirufu wakipiga kura bila vurugu mara baada ya saa
moja asubuhi. Upinzani ulionekana kujiongezea umaarufu katika nyanja
za kisiasa nchini humo.
Chama Kikuu cha Upinzani cha Renamo
kimekuwa kikipambana na chama tawala katika sanduku la kura pamoja na
mapigano ya mara kwa mara ambapo safari hii kiongozi wa Renamo
amejitokeza kutoka mafichoni kushiriki katika uchaguzi huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni