.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Oktoba 2014

LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA, MANCHESTER CITY YAAMBULIA SARE YA MABAO 2-2 DHIDI YA CSKA MOSCOW

Vijana wa Manuel Pellegrin, timu ya soka ya Manchester City wakicheza ugenini mjini Moscow nchini Urusi hii leo wameshindwa kuyalinda mabao yao mawili waliyokuwa wameyapata katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya dhidi ya wenyeji wao CSKA Moscow na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo huo.
Katika mchezo huo, Manchester City walijipatia mabao yao katika dakika ya 29 mfungaji akiwa ni Sergio Aguero huku bao la pili likifungwa na James Milner katika dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza.

Mabao hayo yalidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, lakini kipindi cha pili wenyeji CKSA Moscow walikuja juu na kusawazisha mabao hayo katika dakika za 64 mfungaji akiwa ni Seydou Doumbia na bao la pili likifungwa kwa mkwaju wa penati na Bebras Natcho katika dakika ya 84. 

Hadi mwisho wa mchezo huo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, CSKA Moscow 2 na Manchester City 2.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni