.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Oktoba 2014

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA ZA MIRADI YA VIKUNDI VYA UCHUMI RUVUMA

Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagana na wanavikundi vya uchumi wa Kijiji cha Lugagala wakishangiria ujio wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyefanya ziara ya kukagua miradi ya kiuchumi na maendeleo katika kijiji pao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la msingi la uanzishwaji wa majengo ya vikundi vya uchumi katika kijiji cha Muungano Zomba Mkoani Ruvuma.

Balozi Seif akishiriki kazi za ujenzi wa Taifa katika Kituo cha Afya cha Kijiji cha Lugagala kata ya Kilagano Mkoani Ruvuma.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwapongeza wananchi wa Kijiji cha Lugagala kwenye Mkutano wa Hadhara kwa ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif akiagana na Makamanda wa vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa ndege wa Songea mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Mkoani Ruvuma.
                                                                    
                                                             Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali itaendelea na juhudi zake katika kuona mazao ya wakulima vijijini hasa chakula cha nafaka { Mahindi } yananunuliwa ili kuwaongezea uwezo wa kimapato wakulima hao katika kyukabiliana na ukali wa maisha.

Balozi Seif alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Lugagala kwenye mkutano wa hadhara baada ya kushiriki kazi za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji hicho pamoja na kuweka jiwe la msingi la nyumba za miradi ya vikundi vya uchumi katika Kijiji cha Muungano Zomba akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani Ruvuma kukagua shughuli za kiuchumi, ustawi wa jamii na maendeleo.

Alisema Serikali haiwezi kuona nguvu za Wananchi zina potea bure bila ya kuunga mkono hasa ikizingatia kwamba asilimia 90% ya Watanzania wote wanaishi katika maeneo ya uzalishaji vijijini.

Alifahamisha utafiti na uchunguzi wa kina utafanywa kupitia Halmashauri za Wilaya zinazohusika na uzalishaji wa mazao hayo ya biashara ili kuwadhibiti walanguzi wenye tabia ya kuwanyhonya wakulima kwa ujanja wa kununua mazao yao kwa bei ya chini.

“ Serikali haitokubali kuwaachia walanguzi kuendesha mpango wa kuwanyonya wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei ya chini na wao wakaiuzia Serikali kwa bei ya juu “. Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif alieleza kuwa tathmini itafanywa ili msimu ujao wa kilimo cha nafaka wakulima watendewe na kukamilishiwa haki zao ili kupewa nguvu na ari zaidi ya uzalishaji.

Akizungumza na wana vikundi vya Kijiji cha Lugagala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wananchi wa Kijiji cha Muungano Zomba kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi vitakav yowakomboa kiuchumi hapo baadaye.

Balozi Seif alisema uwamuzi wa wananchi hao kuanzisha vikundi hivyo umekuwa ni jambo la busara wakielewa kwamba suala la ajira ambalo huwakumba zaidi vijana limekuwa gumu hasa katika sekta za umma.

Aliwataka wana vikundi hao lazima wawe makini katika mikutano yao ya tathmini kwa kuondoa urasimu na wawe wazi jambao ambalo litaleta kuaminiana baina ya wana vikundi hao.

Kuhusu suala la Katiba Mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba Balozi Seif alisema viongozi pamoja wabune wenyewe waliousika na mchakato wa kupati,kana kwa Katiba hiyo wataendeleza juhudi katika kuwapatia elimu wananchi kujua faida ya kuipigia kura wakati utapowadia.

Alisisitiza umuhimu wa kudumishwa kwa amani iliyopo Nchini kwa vile makundi yote yaliyoshiriki mchakato huo yameonyesha kuridhika la Katiba hiyo inayopendekezwa.

Balozi Seif aliongeza kwamba wananchi wakati huu wanapaswa kujiepusha na kasumba za upinzani ambazo malalamiko kwao imekuwa ni sehemu ya sera inayopaswa kuachwa na wananchi hao.

Naye Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alihimiza kwamba Kiongozi lazima awe mfano wa maendeleo ya jamii badala ya kushabikia vurugu na siasa chafu.

Mama Asha alisema siasa ni kwa Viongozi kusimamia juhudi na harakati za kiuchumi na maendeleo za wale wanaowaongoza kwa lengo la kuwakomboa kimaisha.

Akitoa Taarifa fupi ya uanzishwaji wa vikundi hivyo vya kiuchumi Afisa Mtendaji wa Kata ya Kilagano Bibi Pulkena Malekela alisema jumla ya vikundi 71 vimeanzishwa katika kata hiyo ili akinamama viwasaidie katika kujikwamua kiuchumi.

Bibi Pulkena alisema kati ya vikundi hivyo 26 viko tayari kut oa huduma vikipata msaada wa uwezeshaji kutoka Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama.

Hata hivyo Afisa Mtendaji huyo wa Kata ya Kilagano alielezea changamoto zinazovikabili vikundi hivyo kwa hivi sasa akizitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa mtaji pamoja na huduma za umeme.

Akitoa msalamu zake mbunge wa Jimbo la Parameho ambae ndie mwenyeji wa ziara hiyo Mh. Jenista Mhagama alisema Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefanya mengi katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Mheshimiwa Jenista Mhagama alieleza kwamba kero nyingi zilizokuwa zikiwakabili wananchi katika sehemu mbali mbali hapa Nchini Mijini na Vijijini zimepungua hasa huduma za maji safi, afya na elimu.

Katika kuunga mkono juhudi za wananchi wa Mkoa wa Ruvuma Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alichangia Shilingi Milioni 1,500,000/- kusaidia Vikundi hivyo pamoja na kuahidi nguvu za uwezekaji kwa majengo ya vikundi hivyo.

Balozi Seif pia akachangia shilingi Milioni 1,500,000/- kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Lugagala pamoja na kuahidi kutoa mifuko mia tano ya saruji ya ujenzi wa kituo hicho.

Othman Khamis Amw
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni