Mwanariadha Oscar Pistorius akiagana na ndugu na jamaa zake baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani na mahakama kuu mjini Pretoria nchini Afrika Kusini hii leo baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kwa kumpiga risasi bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mzunguko mwekundu unaonyesha mduara wa saa ya mkononi aliyokuwa ameivaa mwanariadha huyo kabla ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia. Hapa akiwa ameivua tayari kumkabidhi mmoja wa ndugu zake kabla ya kupelekwa gerezani.
Oscar Pistorius akiagana na mjomba wake Arnod ambaye alikuwa mahakamani kufuatilia hukumu ya kesi yake.
Askari wakimuelekeza mwanariadha Oscar Pistorius kutoka nje ya mahakama tayari kuelekea katika gari maalum lililompeleka gerezani kutumikia kifungo.
Picha juu na chini mwanariadha huyo akipanda gari maalum tayari kupelekwa katika gereza la Pretoria kutumikia kifungo chake.
Dada wa Oscar Pistorius, Aimee akiwa ameshika kichwa chake wakati Jaji Thokozile Masipa akisoma hukumu dhidi ya kaka yake.
Baba mzazi wa Oscar Pistorius, Henke akitoka mahakamani baada ya mwane kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp bila kukusudia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)








Hakuna maoni :
Chapisha Maoni