.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Oktoba 2014

MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO GEREZANI


Mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius raia wa Afrika Kusini amehukumiwa kwenda gerezani miaka mitano ( 5 ) baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kumuua mpenzi wake, mwanamitindo Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi, tukio ambalo lilitokea siku ya wapendanao ( valentine day ) mwaka jana.

Hukumu hiyo ilianza kusomwa asubuhi na kuvuta hisia mbalimbali toka kwa waliokuwa wanaifuatilia kesi hiyo. 

Jaji Masipa alisema kabla ya kutoa hukumu hiyo, changamoto kubwa iliyokuwa inamkabili ni kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote mbili katika kesi hyo.
Mwanariadha Oscar Pistorius akitolewa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni