Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia ramani ya Tanzania
inayoonyesha mchoro wa reli ya Kati inayotarajiwa kujengwa upya na kwa viwango
vya kisasa wakati alipokutana na uongozi wa juu wa makampuni ya China
yakiongozwa na China Railway Group Ltd. Makampuni mengine ni SINOSURE, Exim
Bank, China Development Bank na China Agriculture Development Bank. Rais Dkt.
Kikwete yuko nchini China kwa ziara rasmi ya kikazi.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwenyekiti
wa Kampuni ya China Railway Group Limited Bwana Li Changjin na msafara wake
kuhusu mpango wa serikali ya Tanzania wa kujenga reli mpya na ya viwango vya
kisasa kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma, Tabora kwenda Mwanza, Kaliua kwenda
Mpanda hadi Ziwa Tanganyika. Mazungumzo hayo yalifanyika huko Beijing tarehe
24.10.2014.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni