Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa hatua husika za kutekeleza
upigaji kura ya maoni ya Katiba iliyopendekezwa zimeanza kuchukuliwa
ndani ya serikali na kuwataka wananchi kuwa na subira.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo
Mkoani Tabora wakati akihutubia taifa katika sherehe za kilele cha
mbio za Mwenge zilizoambatana na kumbukumbu ya miaka 15 ya kifo cha
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Dkt. Kikwete amesema ameipitia
vizuri Katiba iliyopendekezwa na kubaini kuwa ni bora na ambayo
imezingatia makundi yote ya jamii wakiwemo wanawake wavuvi na vijana,
hivyo basi anawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya
maoni wakati ukifika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni