Kamati ya dharuza ya Shirika la Afya
Dunia (WHO) inafanya mkutano kuzungumzia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Mkutano huo unaofanyika Geneva
unatathimini hatua za kuimarisha upimaji katika mipaka, na kufikiria
uwezekano wa kuweka utaratimu wenye masharti makali ya kusafiri.
Sheria mpya za Marekani zinawataka
wasafiri kutoka nchi zilizoathiriwa mno na mlipuko wa Ebola kufikia
katika viwanja vitano vya ndege vilivyotengwa kwa ajili yao.
Idadi ya vifo vya ugonjwa wa Ebola
sasa imefikia watu 4,877, ikiwa ni ongezeko la vifo vya watu 322
tangu WHO itoe ripoti yake siku tano zilizopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni