.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Oktoba 2014

SIASA ZA SERBIA NA ALBANIA ZAKATIZA MCHEZO WAO NA KUIBUA NGUMI

Siasa za Serbia zimeathiri mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya Ulaya dhidi ya Albania baada beki Stefan Mitrovic, kuvuta chini bendela iliyokuwa ikirushwa hewani na kifaa maalum na kusababisha vurugu katika dimba la Partizan, na kukamatwa kwa ndugu wa Waziri Mkuu wa Albania.

Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) liliwazuia mashabiki wa Albania kutohudhuria mchezo wa kundi I huko Belgrade lakini waliruhusu mataifa hayo mawili yenye uhasama wa kisiasa kucheza pamoja licha ya mgogoro wao wa muda mrefu.

Bendera hiyo ya Albanian iliyokuwa na ramani ya Kosovo pamoja na ujumbe 'autochthonous', ukiwa na maana ya wazawa, ambapo kitendo cha Mitrovic kuirukia bendera hiyo na kukishusha chombo kilichokuwa kikiongozwa na remoti kuipeperusha bebdera hiyo kilichafua hali ya hewa.
        Ugomvi ukiendelea dimbani huku shabiki akimpiga na kiti mchezaji
Bendera ikipeperushwa dimbani na chombo maalum
 Mitrovic akiirukia bendera hiyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni