.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Oktoba 2014

WANAJESHI SABA WA AFGHANISTAN WAFARIKI DUNIA BAADA YA MSAFARA WAO KUSHAMBULIWA KWA BOMU

Mpaka sasa imethibitishwa wanajeshi 7 wa Afghanistan wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa baada ya msafara wao kushambuliwa kwa bomu lililokuwa limelengwa kushambulia basi walilokuwa wakisafiria wanajeshi hao mjini Kabul. 

Basi la pili nalo lilishambuliwa na bomu na kujeruhiwa wanajeshi wawili na raia wawili. Kundi la kigaidi la Taliban wametangaza kuhusika katika matukio hayo mawili. 

Mashambulio hayo yamekuja ikiwa ni siku moja tu kupita tangu maofisa wa Afghanistan na Marekani wasaini makubaliano ya Majeshi ya Marekani kuendelea kusalia nchini humo hata baada ya mwaka huu wa 2014

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni