.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 14 Novemba 2014

JENGO LA MACHINGA COMPLEX LINAWAKA MOTO

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa jengo la wafanyabiashara ndogo ndodo maarufu kama Machinga Complex ambalo lilpo wilaya ya Ilala katika jiji la Dar es Salaam linawaka moto. 

Taarifa zinasema kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, ila moto huo umeanzia katika moja ya vyumba vilivyopo ghorofa ya juu. 

Hata hivyo vikosi vya ulinzi na usalama vimewahi kufika eneo la tukio kudhibiti amani huku vikosi vya zimamoto vikiendelea kuwasili eneo hilo kwa ajili ya kuuzima. 

Foleni ya magari ni kubwa kuanzia makutano ya barabara karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja na ile ya kutoka makutano ya Chang'ombe. Haya ni yale magari yanayopita karibu na jengo hilo.

Nao wafanyabiashara hao " wamachinga " wameonekana kujitahidi kuokoa mali zao. Tutawapa taarifa zaidi na picha hapo baadaye.
Muonekano wa jengo la Machinga Complex linavyoonekana toka kwa nyuma katika uwanja wa Karume.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni