.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Novemba 2014

LIGI KUU UINGEREZA, CRYSTAL PALACE YAITANDIKA LIVERPOOL 3-1

Pamoja na kutangulia kupata bao la mapema katika dakika ya pili tu ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Rickie Lambert, Liverpool imejikuta ikiambulia kipigo cha mabao 3-1 toka Crystal Palace katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliochezwa leo. 

Wakicheza nyumbani, Crystal Palace baada ya kufungwa bao hilo walijpanga na kuanzisha mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Liverpool. 

Mashambulizi hayo yalizaa mabao kupitia kwa Dwight Gayle aliyefunga bao la kusawazisha katika dakika ya 17, bao la pili likifungwa na Ledley katika dakika ya 78 na bao la 3 nala ushindi likifungwa na Mile Jedinak kunako dakika ya 81.
Mambo magumu msimu huu hadi namkumbuka Suarez!! Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers akiwa mnyonge baada ya timu yake kuchapwa 3-1.
Hata mimi kiduku nakiweza!! Kocha wa Crystal Palace, Neil Warnock akifurahia matokeo hayo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni