.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Novemba 2014

LIGI YA MABINGWA ULAYA, CHELSEA YAIFUMUA SCHALKE 5-0, CSKA NA ROMA NGOMA DROO, PSG YAICHAPA AJAX 3-1

Imethibitika kuwa, ukali wao sio katika ligi kuu nchini Uingereza pekee bali hata katika ligi ya mabingwa barani Ulaya. 

Matajiri wa london Chelsea usiku wa kuamkia leo wakicheza ugenini dhidi ya Schalke ambayo sasa inanolewa na Roberto Di Mateo aliyepata kuifundisha Chelsea na kuipa ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya, wameibuka na ushindi wa mabao 5-0.
Katika mchezo huo ambao Chelsea waliutawala na kuwachanganya kabisa Schalke, walijipatia mabao yao kupitia kwa nahodha John Terry, Didier Drogba, William na Ramires huku mchezaji wa Schalke Jan Kirchhoff akijifunga bao wakati akiwa katika harakati za kuondoa hatari langoni mwake.
Mashabiki wa Schalke wakiondoka mapema uwanjani baada ya kushuhudia timu yao ikipewa adhabu ya kufungwa mabao 5-0 na Chelsea katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo. 

Matokeo mengine ya michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo:-

CSKA Moscow 1 vs 1 Roma

Paris St Germain 3 vs 1 Ajax

Sporting 3 vs 1 NK Maribor

BATE 0 vs FC 3 Porto

Shaktar 0 vs 1 Athletico Bilbao 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni