Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kampuni ya New Habari ( 2006 ) Ltd, Innocent Munyuku ( 41 ) aliyefariki dunia usiku wa kumakia juzi unaagwa leo katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Travena Mwaimu ilisema mwili wa Munyuku utaagwa kuanzia saa nne asubuhi.
Alisema baada ya taratibu za kutoa heshima za mwisho kukamilika, mwili huo utasafirishwa kwenda Mazimbu mkoani Morogoro kwa maziko yatakayofanyika kesho
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni