.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 21 Novemba 2014

MWANDISHI MUNYUKU KUAGWA LEO HOSPITALI YA LUGALO, BARAKA KARASHANI KUZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KESHO

Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mwili wa mwandishi wa zamani wa michezo, Innocent Munyuku aliyefariki dunia juzi, unaagwa leo Ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Morogoro kwa mazishi.
 

Pia mwili wa mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani, aliyefariki juzi utazikwa kesho Jumamosi makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam badala ya leo makaburi Sinza kama ilivyokuwa imetangazwa jana. 

Msiba upo nyumbani kwa wazazi wa marehemu maeneo ya Mawasiliano Tower, barabara ya Sam Nujoma, Ubungo Dar es Salaam.
 

                                                                                             Nawasilisha,
                                                                                   Katibu Mkuu TASWA
                                                                                             21/11/2014

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni