Mamia kwa maelfu ya wananchi wa
Uswizi wanakula nyama za paka na mbwa, ambapo wanaharakati wanataka
ulaji wanyama hao upigwe marufuku nchini humo.
Wanaharakati hao wamekusanya saini
16,000 na kuzikabidhi kwa bunge la nchi hiyo ili kutunga sheria ya
kuwazuia watu kula wanyama hao wa nyumbani.
Muasisi na Rais wa Taasisi ya
Kulinda Wanyama Tomi Tomek, amesema robo tatu ya raia wa Uswizi
wanakula wanyama hao, ambapo nyakati za krismasi wanyama hao huwa mlo
muhimu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni