Polisi nchini Marekani wamesema
mwanaume aliyewauwa kwa kuwapiga risasi maafisa polisi wawili, Jijini
New York aliwaambia watu waangalie kile anachoenda kukifanya muda
mfupi, kabla ya kufanya shambulio hilo.
Mtu huyo Ismaaiyl Brinsley, 28,
anarekodi za kufanya fujo, pia inasemekana anamatatizo ya akili.
Brinsley aliwapiga risasi maafisa
polisi hao waliokuwa wamekaa kwenye gari la polisi la dori eneo la
Brooklyn kabla ya kukimbilia kwenye njia ya treni ya aridhini na
kujiua kwa kujipiga risasi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni