.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Desemba 2014

LIGI KUU UINGEREZA, LIVERPOOL CHUPU CHUPU KULALA NYUMBANI DHIDI YA ARSENAL

 Liverpool imeponea chupu chupu kulala katika uwanja wake wa nyumbani " Anfield " baada ya kupambana kiume na kulazimisha matokeo kuwa 2-2 hadi mpira unamalizika dhidi ya wageni wao Arsenal. 

Katika mchezo huo wa ligi kuu nchini Uingereza uliokuwa na ushindani mkali, Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Coutinho katika dakika ya 44. 

Hata hivyo Arsenal walisawazisha bao hilo katika dakika ya 45 kupitia kwa Debuchy katika dakika ya 45.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kusaka mabao zaidi, ndipo Giroud alipoifungia Arsenal bao la pili katika dakika ya 64. 

Mchezo ukionekana kama Arsenal wanaoondoka na ushindi, ndipo Skrtel alipojikunja na kupiga kichwa safi na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 90 hivyo kufanya matokeo kuwa 2-2- hadi mpira unamalizika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni