Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI)
Dkt. Shija Kazumba (kushoto) akimkaribisha Mgeni rasmi katika maafali ya sita
ya Taasisi hiyo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mgeni rasmi wa mahafali
hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwahutubia wahitimu (hawapo pichani)
wakati wa mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI).
Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Dkt. Shija
Kazumba na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Prof. Gabriel Roderick
Kassenga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea risala ya wahitimu iliyosomwa na
kuwasilishwa kwa mgeni rasmi na Bw. Magembe Maduhu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimpa tuzo mhitimu aliyeongoza katika kundi
la wanawake na aliyekua na ufaulu mkubwa kuliko wahitimu wote Bi. Fatma Ngano,
kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Dkt. Shija na
ushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Prof. Gabriel Roderick Kassenga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo ambaye pia ni mgeni rasmi katika mahafali ya sita ya Taasisi ya
Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye
miwani) katika picha ya pamoja na wakufunzi na wahitimu wa Taasisi hiyo.
Kikundi cha ngoma kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania Mwenge
wakitumbuiza wakati wa mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa
Maji (WDMI) yaliyofanyika hivi karibuni.
Picha na: Genofeva
Matemu – Maelezo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni