.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 19 Desemba 2014

TUZO ZA BODI BORA KATIKA SEKTA ZA KIBENKI NA BIMA KUFANYIKA MWEZI UJAO


TUZO za Bodi yenye Uongozi Bora ijulikanayo kama Best Board Leadership Award (BBLA), ambazo zimelenga kutambua uongozi bora wa Bodi za Wagurugenzi katika sekta ya kibenki na bima, zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi ujao. BBLA iliyopangwa kufanyika mwezi Januari tarehe 30 na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini, inaandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI).

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa BBLA Bi. Neema Gerald alisema tuzo hizo zinatoa fursa ya ufahamu wa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo walilobobea kiutalaam.

Wadhamini wa tukio hilo la kipekee ni pamoja na Capital Plus Internaional Limited, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel na IPP Media, wakati wadhamini wengine wakiaswa kujitokeza zaidi kuunga mkono tuzo hizo.

"Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao.Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizo ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakuwazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, "alisema.

Bi. Neema alisema kuwa utamaduni unaojulikana ni kuwa ni Maafisa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi Wakuu pekee ndiyo wanaothaminiwa na kutambuliwa na waajiriwa au jamii nzima kwa ujumla. 

"Ni wakati muafaka sasa kwa bodi zenye utendaji bora kutambuliwa na kuzawadiwa kikamilifu kwa jitihada zao," alisema. Alibainisha kuwa zoezi hilo, tathmini na upangaji wa mwisho wa matokeo utafanywa na jopo la majaji waliobobea na wenye rekodi bora za kiutendaji.

Tathmini hiyo italenga zaidi katika ufanisi wa Bodi ya Wakurugenzi katika suala la utawala wa taasisi, usimamizi wa fedha na uwezo wa kuiongoza dira ya taasisi kwa ujumla wake. Maeneo mengine ni umakini wa bodi katika uwazi, uwajibikaji, utendaji, na ufuataji wa hatua madhubuti na  utendaji wake.

Alitaja maeneo mengine ambayo bodi itafanyiwa tathmini kuwa ni utoaji wa mitazamo yakinifu ya bodi katika kusisitiza umuhimu wa utendaji wa mtaji watu katika ngazi ya bodi na kuweka mbele vigezo vitakavyowezesha utendaji bora zaidi wa bodi, "alisema.

Aliongeza kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa wakati muafaka nchini wakati ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa na kujitokeza kwa makampuni mengi ya bima na masoko zaidi kuongezeka ili kufikia wateja wengi katika nyanja zote za maisha.

"Kwa mabadiliko haya wakati huu, hasa katika sekta ya fedha ambapo idadi kubwa ya makampuni ya bima na mabenki zimekuwa zikifungua biashara Tanzania, wateja wanahitaji kuwa na uhakika kuwa malipo yao ya bima yako salama na wanaweza kupatiwa kwa wakati wowote", alisema, na kuongeza:

"Hili litafanikiwa tu endapo kampuni hiyo ya bima au benki itaendelea kufanya kazi kwa mafanikio. Kwa maana hiyo, bodi ya wakurugenzi itakuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha kampuni hiyo haifi, "alisema.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni