.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 11 Januari 2015

LIGI KUU UINGEREZA, CHELSEA YAENDELEA KUIKIMBIA MANCHESTER CITY

Vinara wa ligi kuu nchini Uingereza, Chelsea jana waliendelea kukaa kileleni baada ya kuitungua Newcastle kwa idadi ya mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini humo. 

Mshambuliaji kinda raia wa Brazil, Oscar ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipatia Chelsea bao la kuongoza katika dakika ya 43 na bao la pili likiwekwa kimiani na mshambuliaji mwenye uchu wa mabao, Diego Costa katika dakika ya 59. 

Kwa matokeo hayo, Chelsea inaendelea kuongoza ligi kwa kuwa na pointi 49.
Wao mabingwa watetezi wa kombe hilo, Manchester City walijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Everton waliokuwa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani. 

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu hizo zilikuwa hazijafungana, na bao la kipindi cha pili kutoka kwa Fernandinho katika dakika ya 74 liliwafanya Manchester City wadhani wangeondoka na ushindi ugenini.

Lakini bao la kusawazisha la Everton toka kwa Steven Naismith dakika ya 78 lilifanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1. 

Man City wameendelea kuwa nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 47.
Pamoja na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland, Liverpool wamefikisha pointi 32 na kusimama katika nafsi ya nane katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza. Katika mchezo huo wa ligi kuu uliochezwa jana, bao la Liverpool lilifungwa na Lazar Markovic katika dakika ya 9 ya mchezo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni