.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Januari 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA MJINI ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakiwa katika Sala na Dua ya kumuombea aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali kabla ya mazishi yake iliyofanyika leo Januari 08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali Jang’ombe Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakisaidia kutoa nje ya msikiti Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali baada ya Sala na Dua maalum iliyofanyika leo Januari 08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali Jang’ombe Zanzibar.
Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali kuelekea katika makaburi ya Mwanakwerekwere Zanzibar kwa ajili ya mazishi leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Udongo kwenye Kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo Januari 08,2015 katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar. Picha na OMR

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni