Wachezaji wa timu ya Yanga wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Shaba kabla kuaza kwa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. Katika mchezo huo Yanga imeshinda bao 1-0.
Kikosi cha Timu ya Shaba (Wazee wa Dago) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza mchezo wao na Yanga kukamilisha ratiba ya Kombe la Mapinduzi hatua za makundi, ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Yanga.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga kutoka Brazil Countinho, akishangilia bao lake alilofunga katika kipindi cha pili dakika ya 86 ya mchezo huo akiwa na mchezaji mwezake kutoka Laiberia. Timu ya Yanga imeshinda bao 1-0, dhidi timu ya Shaba Wazee wa Dago kutoka Micheweni Pemba. Kwa hisani ya ZanziNews
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni