.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 30 Januari 2015

SHAHIDI ADAI NAIBU RAIS KENYA ALICHOCHEA WAKALENJINI KUWAUWA WAKIKUYU

Shahidi amedai kuwa Naibu Rais wa Kenya William Ruto aliichochea jamii ya kabila la Kalenjin kuwauwa watu wa kabila la Kikuyu katika machafuko yaliyotokea kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.

Shahidi huyo ameiambia mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), kuwa Ruto aliwachochea wakalenji kuwafukuza wakikuyu katika mkoa wa Bonde la Ufa, iwapo chama chake ODM hakitashinda uchaguzi wa mwaka 2007.

Hata hivyo wakili wa Ruto, alipinga madai hayo na kusema ni ya uongo na yaliyotungwa dhidi ya mteja wake. Ruto na mtangazaji Joshua arap Sang wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu walioutenda wakati wa ghasia za uchaguzi za mwaka 2007-2008.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni