.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Januari 2015

WATU WENYE SILAHA WAUA WATU 12 KATIKA OFISI YA MAJARIDA NCHINI UFARANSA

Wanaume wawili wenye silaha wameishambulia kwa risasi ofisi ya kuchapisha majarida ya Charlie Hebdo nchini Ufaransa na kuua watu 12 na kuwajeruhi wengine saba.

Watu hao ambao ni waislamu wenye itikadi kali walifyatua risasi katika ofisi hiyo wakitumia silaha aina ya rifle na kisha kupambana kwa kutupiana risasi na polisi mtaani kabla ya kutoroka kwa gari.

Mashahidi wamesema watu hao wenye silaha walisikika wakipaza sauti zao wakisema tunalipa kisasi kwa ajili ya mtume Mohammad.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema bila shaka hili ni shambulio la kigaidi linaloonyesha unyama usiowakawaida.
                     Mmoja wa majeruhi akitolewa katika ofisi iliyoshambuliwa kwa risasi 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni