Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akiongea na bodi na menejimenti ya mamlaka maji jiji la Mbeya baada ya Naibu waziri huyo kutembelea mamlaka ya maji safi jijini Mbeya. Aidha aliipongeza mamlaka hiyo kwa kuongeza wateja kutoka 9000 mwaka 2002 na kufikia 40,000.
Mh Makall pia aliipongeza kwa kuwa mamlaka ya tatu kitaifa kuwa na miundombinu ya majita, huku pia akiiagiza kudhibiti upotevu wa maji kutoka asilimia 34 ya sasa na wafikie kiwango cha kimataifa asilimia 20.
Mh Makalla amezitaka mamlaka zingine kushirikiana na mamlaka kutokutoa vibali vya makazi eneo la vyanzo vya maji na pia amewataka wananchi kutunza, kutolima, kukata miti na kuchafua vyanzo vya maji
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni