.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Januari 2015

ZOEZI LA KUTAFUTA KISANDUKU CHA BLACK BOX CHA AIRASIA LAANZA TENA

Zoezi la kutafuta kisanduku cha kurekodi taarifa cha ndege ya abiria iliyoanguka ya AirAsia, limeanza wakati hali ya hewa ikianza kuboreka katika bahari ya Java.

Ndege hiyo namba QZ8501 ilikuwa ikitokea Surabaya, Indonesia kwenda Singapore Desemba 28, ikiwa na abiria 162 kabla ya kutoweka kwenye rada.

Msako umefanikiwa kupata miili 37 hata hivyo mabaki ya miili ya wahanga wa ajali hiyo inaaminika kuwa bado ipo ndani ya ndege chini ya bahari.

Hali mbaya ya hewa imekwamisha jitihada za wazamiaji kufikia kitu kimoja kikubwa kinachohisiwa kuwa ni mabaki ya ndege hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni